Baada ya maagizo ya JPM, Mkurugenzi Ubungo anena
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic, amesema kuwa ameyapokea maagizo ya Rais Magufuli, na kwamba walikwishaanza kuchukua hatua za ujenzi wa shule ya msingi King'ong'o ikiwemo kutenga milioni 80, baada ya wao kuona video ikionesha changamoto ya shule hiyo.