Polisi yaelezea suala la Lema kutishiwa maisha
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Salum Hamduni, amesema kuwa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, hajawahi kutoa taarifa kama anatishiwa maisha na wala hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtishia maisha yake.