"Bunge hili litahukumiwa"-Spika Ndugai
Spika wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa atahakikisha taarifa zote sahihi za Bunge hilo zinawafikia wananchi ili isije ikaonekana Bunge hilo halifanyi kazi na halisikiki kwa sababu wabunge wengi waliomo ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM).