
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.
Spika Ndugai, ametoa kauli hiyo leo Novemba 10, 2020, mara baada ya kula kiapo cha kuendelea kushika nafasi hiyo, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwapa usia wabunge kuwa, wajitahidi kuzungumza na wasiwe mabubu kwa manufaa ya wananchi wao waliowapigia kura.
"Tutajitahidi katika Bunge hili taarifa nyingi za Bunge zinawafikia wananchi, tukijifungia hapa habari zisiwafikie wananchi, Bunge hili litakuwa limehukumiwa toka mwanzo kwa kuwa lina wabunge wengi wa CCM ndiyo maana halisikiki, halifanyi kazi na halionekani, lazima Bunge hili lionekane, lisikike linavyoishauri na kuiambia serikali", amesema Spika Ndugai.