EWURA yaingia makubaliano na LATRA
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (EWURA) imesaini mkataba wa makubaliano na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) wenye lengo la kufanya kazi pamoja ili kusaidia kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo udhibiti wa mafuta na usafirishaji.