Monday , 16th Nov , 2020

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (EWURA) imesaini mkataba wa makubaliano na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) wenye lengo la kufanya kazi pamoja ili kusaidia kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo udhibiti wa mafuta na usafirishaji.

Kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe na kulia ni watumishi kutoka EWURA

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo Jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, EWURA, Bw. Ahmad Kilima, amesema mkataba huo utasaidia kuweka mikakati mbalimbali itakayosaidia kutoa elimu kwa umma na kusaidia kupunguza ajali na kuweka usalama wa watu na mazingira.

Ameongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mamlaka na taasisi mbalimbali za serikali kuungana na kushirikiana katika utoaji wa huduma zao ili kuweza kufika mbali na kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuongeza uaminifu kwa wadau.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe amesema watahakikisha wanaongeza udhibiti wa magari mabovu yanayobeba mnafuta ili kuuondoa changamoto ya uchakachuaji mafuta njiani.