RC Makonda kuanza msako jijini Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema kuanzia Jumatatu ya June 3, 2019 ni marufuku kwa mfanyabiashara yeyote mdogomdogo (machinga) ndani ya mkoa huo kufanya biashara bila vitambulisho maalumu vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.