Mwigulu akiri kufurahishwa, amshukuru JPM
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dk. Mwigulu Nchemba ametembelea kukagua ujenzi wa nyumba za polisi Mkoani Arusha ambazo ziliungua kwa ajali ya moto iliyotokea mwaka jana ambapo amekiri kufurahishwa na kuridhishwa na hatua za ujenzi zilipofikia.

