Rufaa za Mikopo ya chuo zafanyiwa kazi
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Disemba 5, 2017) imetangaza orodha yenye wanafunzi 2,679 ambao wamepata mikopo ya elimu ya juu yenye thamani ya TZS 9.6 bilioni kufuatia kukamilika kwa uchambuzi wa rufaa zilizowasilishwa.