"Mr. Nice ni mahututi" - Dudu Baya
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mkongwe, Godfrey Tumaini au Dudu Baya, ameshangazwa na kitendo cha msanii mwenzake Lucas Mkenda au Mr. Nice kusema anataka kumsaidia kimuziki, wakati mwenyewe yuko taaban hajiwezi.