Maxime atamani kuinoa Stars
Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, na Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema Stars inahitaji kocha ambaye ana uwezo wa kutambua wachezaji wenye vipaji, malengo na moyo wa kujituma ambao wataisaidia timu hiyo kusaka matokeo mazuri.

