Mzee Akilimali azidi kumchana Niyonzima
Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali amesema hawana wasiwasi wowote juu ya kuondoka kwa kiungo wao Niyonzima kwa kuwa wapo wengi walishaondoka waliokuwa wazuri katika timu yao akiwamo Sunday Manara na timu iliendelea kufanya vizuri.

