"Membe hajauawa ni kifo cha kawaida" - Daktari
Daktari wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Bernard Membe, ameondoa sintofahamu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe na kusema hajauawa bali kifo chake kimetokana na maambukizi ya ghafla ya mapafu yaliyopelekea damu kuganda.