Serikali yasaka teknolojia ya kukaushia nafaka
Serikali imesema imejizatiti katika kuwaandaa na kuwatafuta wataalam wa kilimo hasa wenye uwezo kuhusu maswala ya ukaushaji wa mazao ya nafaka ili kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na tatizo la unyevunyevu kwenye mazao hayo.