Wananchi washauriwa kutoa maeneo bila fidia
Wakazi mkoani Kagera hasa katika Manispaa ya Bukoba wametakiwa kutoa maeneo yao bila kudai fidia ili kuruhusu Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kupitisha nguzo za umeme, lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma hiyo kwa gharama nafuu ya shilingi 27,000.