Watahiniwa 2,194 wafutiwa matokeo yote
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 2194 sawa na asilimia 0.16 ya watahiniwa milioni 1.35 waliofanya mitihani, baada ya kubainika wamefanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022.