Wakimbizi kutoka Burundi wagoma kurudi kwao
Asilimia 95 ya Wakimbizi na waomba hifadhi wa nchi ya Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu Wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamegoma kurejea nchini kwao, kwa kile wanachodai bado hali ya amani hairidhishi