Thursday , 29th Dec , 2022

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii  imepanga kutoa hekari 2500 ya Hifadhi ya Msitu wa Ndechela ulioko wilayani Nanyumbu ili zitumike na wanakijiji wa Mkopi kwa shughuli mbalimbali za kijamii.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana,

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, mkoani Mtwara kwenye ziara ya kamati ya mawaziri nane wa kisekta inayoshughulikia migogoro ya ardhi nchini.

Mhe. Balozi Dkt. Chana amesema licha ya tafsiri ya kisheria kuonesha kuwa wananchi wamelifuata eneo hilo busara za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeona iachie eneo hilo la hifadhi litumiwe na wananchi.

Aidha Waziri Balozi Dkt. Chana ameendelea kutoa wito kwa jamii iendelee kuungana na serikali katika kulinda maeneo ya yaliyohifadhiwa ili yatumike kwa faida ya watanzania wote pia akikemee tabia ya baadhi ya watu wachache wanaovamia maeneo hayo kuanzisha shughuli za kibinadamu zikiwemo za kilimo na ufugaji.