Viongozi waonywa ubadhilifu wa fedha
Serikali Mkoani Geita imewataka viongozi wa jumuiya za maji kuacha ubadhilifu wa fedha wanazokusanya kwenye uuzaji wa maji badala yake wawe waadilifu kwenye ukusanyaji na matumizi sahihi ili kila mwananchi aweze kunufaika na uwepo wa miradi ya maji kwenye eneo lake.