Twiga Stars yaichapa Zambia Shepolopolo 4-2
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la wanawake Twiga Stars imeanza vema kampeni yake ya kufuzu kwa fainali za michuano ya All African Games, baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 4-2 katika ardhi ya ugenini dhidi ya wenyeji Zambia.