Minja waambie wadau wasifunge maduka -Mahakama
Hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Dodoma Rebecca Mbilu amemtaka mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabishara nchini, Johnson Minja kuwaambia wafanya biashara nchini waache kufunga maduka yao wakati wa kesi yake kwani ni sharti mojawapo la dhamana yake.