Amchinja mke wake kisa mapenzi
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linamshikilia Mapinduzi Siliya (45), mkazi wa Nzovwe, kwa tuhuma za kumuua mke wake Terezia Mtajiha, kwa kumchinja na kisu shingoni kisha kwenda kuutupa mwili wake Mto Nzovwe, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

