Makazi yazingirwa na tope chafu la mgodini
Bwawa la maji machafu katika mgodi wa Williamson Diamond wa mkoani Shinyanga, limepasuka na tope kutiririka kwenye makazi ya watu na kusababisha nyumba 13 kuzingirwa na tope na maji machafu huku wakazi wakilazimika kuyahama makazi yao kwa muda kwa ajili ya usalama.