Wafanyabishara waangua kilio kuhamia Mbagala
Wafanyabiashara wa soko la wakulima la Nyankumbu Halmashauri ya mji Geita, wameugomea uongozi wa Halmashauri hiyo uliowataka kuhama ndani ya siku tatu kwenye soko hilo na kwenda soko la Mbagala ambalo wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilikimbia kutokana na kutokuwa na wateja.