Waziri Mkuu atoa maagizo Wizara ya Maji
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji kwa kushirikiana na sekta binafsi ihakikishe inakamilisha taratibu za utekelezaji wa mradi wa kutoa maji mto Rufiji utakaosambaza maji katika maeneo ya mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.