Haaland yupo fiti kuwavaa Watakatifu Soton
Mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland yuko tayari kuwakabili Southampton Jumamosi hii. Nyota huyo alikuwa nje ya uwanja tangu mwezi Machi baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Bournemouth.