Jumanne , 4th Oct , 2022

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP) imekabidhi Wizara ya Fedha na Mipango mali 8,188 zenye thamani ya billion 4.4 zilizotumika kutenda uhalifu mbalimbali nchini.

Katibu wa Wizara ya Fedha na Mipango dkt Emmanuel Tutuba(Kushoto mwenye miwani)akipokea ripoti ya mali zilizotumika katika uhalifu kutoka kwa DPP.

Akizungumza katika Hafla ya makabidhiano ya mali zitokanazo na uhalifu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  jijini Dodoma,katibu mkuu wizara ya fedha na Mipango Emmanuel tutuba ametoa wito kwa watanzania kuzingatia sheria na kutojiingiza kwenye vitendo vya kihalifu kwani vinaweza kuhatarisha Maisha yao na utajiri wao. 

"watanzania zingatieni sheria na msijiingize kwenye vitendo vya kihalifu maana sheria ipo wazi na kama umetoa gari kumpa mtu ufahamu linaenda kutumika kwa shughuli gani na lisije kutumika kwenye vitendo viovu badae likakuletea hasara" Amesema Tutuba.

sambamba na Hayo Tutuba amesema baada ya kukabidhiwa mali hizo watafanya uchambuzi kuona zinazofaa kwa ajili ya matumizi ya Serikali na watazigawa kwa taasisi za umma zikaendelee kutoa huduma mbalimbali za kijamii na zingine zitapigwa mnada.