Alhamisi , 11th Mei , 2023

Meneja wa Wakala wa Vipimo katika Jiji la Ilala Alban Kihula amesema kwa mujibu wa sheria mfanyabiashara yoyote anayetumia mizani kupima bidhaa anapobainika amechezea mizani ili kupunguza kiwango halisi atalazimika kulipa faini ya kuanzia shilingi laki moja mpaka shilingi milioni 20

Amesema pia anaweza kufikishwa mahakamani na kutozwa faini ya shilingi laki tatu mpaka shilingi milioni 50
Akizungumza na EATV leo Meneja huyo amesema suala la wafanyabiashara kuchezea mizani limekuwa ni changamoto kubwa hapa nchini na kusababisha malalamiko mengi kwa wananchi kupunjwa bidhaa wanazonunua maeneo mbalimbali

Hata hivyo EATV imefikia mpaka kwa wafanyabiashara wa nafaka na bucha za nyama ambao ndio wamekuwa wakilalamikiwa zaidi ambapo wamesema licha ya kukiri kuwepo kwa tabia hiyo lakini mara baada ya kuelimisha na kufahamu sheria za makosa hayo wengi wao wameachana na tabia hiyo

Nao wananchi waliofika kununua nyama na nafaka katika maeneo hayo wameeleza uelewa wao wa kutambua iwapo bidhaa aliyonunua ipo kwenye kipimo halisi Ili kuepuka kupewa bidhaa iliyo pungufu na mahitaji yake mara baada ya kuelimisha