Jumanne , 4th Oct , 2022

Viongozi wa chama cha wamachinga mkoa wa Dar es salaam wametaka kukomeshwa mara moja kwa makundi ya kihalifu maarufu kama Panyaroad ambapo wamesema baadhi ya wamachinga wamekuwa ni wahanga na makundi hayo na hivyo kuwarudisha nyuma kiuchumi

Wakizungumza na waandishi wa habari leo mwenyekiti wa wamachinga mkoa wa Dar es salaam Namoto Yusuph Namoto licha ya kulipongeza Jeshi la polisi kwa jitihada zake za kupambana na makundi hayo ya kihalifu lakini wametoa wito kwa jamii na wanasiasa kuacha siasa chafu ambazo zitaathiri maana nzima ya Jeshi la polisi katika kusambaratisha makundi hayo

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa wamachinga Steven Simbo amewashauri vijana wanaofanya uhalifu kuacha mara moja na badala yake kwenda kwenye soko hilo kutafuta fursa za kufanya biashara kwani wapo vijana ambao walikuwa wahalifu lakini Kwa sasa waneungana na wenzao kufanya biashara ndogondogo na kuachana na uhalifu

Naye Bakari Said Mkupa ambaye ni mwenyekiti wa wamachinga wilaya ya Ilala ameitoa hofu serikali kwamba panyarroad hawawezr kujichanganya na wafanyabiashara hao Ili kufanya uhalifu kwa kuwa tayari wana kanzi data inayowatambua wafanyabiashara hao hivyo haitakuwa rahisi kufanya uhalifu