Jumatatu , 28th Nov , 2022

Mamlaka nchini  Cameroon  imesema kwamba Maporomoko ya ardhi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Yaoundé, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 14,

Waliopoteza maisha kwenye maporomoko hayo walikuwa wakihudhuria mazishi, kulingana na gavana wa eneo hilo, Naseri Paul Bea.

Vikosi vya uokozi vilikuwa bado vinatafuta miili na manusura Jumapili jioni.Wakazi wamesema familia kadhaa za waombolezaji zilikusanyika chini ya mahema makubwa kwenye yaliyokua kwenye milima , wakati sehemu ya ardhi ilipogawanyika mara mbili na kuwafukia chini.

Hilo ni janga la hivi karibuni linalohusiana na hali ya hewa nchini Cameroon mwaka huu. Waandishi wa habari wanasema mvua kubwa imesababisha mafuriko kadhaa mabaya kote nchini Cameroon mwaka huu, na kudhoofisha miundombinu na kuwakosesha makazi maelfu ya wakaazi.