Jumamosi , 25th Dec , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewatakia heri za sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, Watanzania wote  na kuwataka kusherehekea kwa amani na utulivu na kusisitiza umoja kwa mwaka 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Heri hizo amezitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, hii leo Desemba 25, 2021, ikiwa Tanzania na Mataifa mengine yakisherehekea sikukuu hii ya kuzaliwa kwa Kristo.

"Nawatakia Watanzania wote heri ya Krismasi na Mwaka Mpya, tusherehekee kwa furaha, amani, utulivu na kiasi, tuendelee kuwa wamoja katika mwaka 2022, tukifanya kazi kwa weledi wa hali ya juu, kwa uzalendo na kwa nidhamu, ili tuendelee kupiga hatua mbele zaidi kimaendeleo," ameandika Rais Samia