Dkt. Philip Mpango amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara Jijini Dodoma leo ambapo amesema hiyo itaepusha kuvujisha siri za Serikali.
“Wakuu wa Wilaya mnapaswa mzingatie kuwa siri ndio uhai wa Serikali hivyo ni lazima mdhibiti uvujaji wa siri za Serikali, epukeni kabisa kutumia mitandao ya kijamii kama WhatsApp au Email binafsi kutuma nyaraka za Serikali”




