Alhamisi , 6th Oct , 2022

Takribani watu 31 wameuawa  kutokana na shambulizi la kisu na risasi lililofanywa na askari polisi wa zamani huko nchini Thailand , kwenye shule ya watoto wadogo.

 Polisi wa nchi hiyo wamesema kwamba msako wa mtuhumiwa huyo unendelea katika jimbo la Nong Bua Lamphu lililopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. 

Polisi wamesema kuwa waliouawa ni pamoja na watoto wadogo na watu wazima. Mshambuliaji huyo alikua akifyatua  risasi na kuwachoma visu watoto , ambapo amekimbia baada ya tukio hilo na kwamba haijulikani sababu ya kufanya hivyo. 

Hata hivyo ilikuja kugundulika kwamba mtuhumiwa huyo aliamua kujiua baada ya kumuua mke na mtoto wake mdogo.

Taarifa kutoka Thailand zinasema kwamba afisa huyo wa polisi aliachishwa kazi siku za  nyuma sababu ya dawa za kulevya.

 Mkuu wa polisi katika jimbo la Nong Bua Lamphu amesema kuwa watoto 23 ni miongoni mwa waathiriwa wa tukio hilo. Matukio ya mauaji ya halaiki ni nadra kutokea nchini humo, ambapo mwaka  2020 askari mmoja aliwaua watu 21 na kujeruhi wengine katika jiji la Nakhon Ratchasima.