Jeneza lililobeba mwili Consolanta Charles
Imeelezwa kuwa vipimo vya awali vya hospitali vilionesha kuwa mtoto huyo alikuwa na Malaria pamoja na UTI na alipewa rufaa ya kwenda hospitali kubwa lakini alirudi nyumbani na ndipo mlezi wake alipoamua kumpeleka kwa mchungaji kwa ajili ya maombi.
Mlezi wa mtoto huyo pamoja na ndugu na majirani wa marehemu wamesema kwa mara kadhaa mtoto huyo alilazwa hospitali na baadaye kuruhusiwa kurudi nyumbani na baada ya muda hali yake ilirudi na kuamua kumpeleka kwa mchungaji kwa ajili ya maombi.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Mkuyuni Gitani Chembanengi, amethibisha kutokea kwa kifo hicho cha mtoto Consolanta na tayari akiwa amezikwa kijijini hapo.




