
Kwa mujibu Mkuu wa Mkoa wa huo Albert Chalamila aliwataka wafanyabaiashara hao kuhama kwenye maeneo ambayo yanatajwa si rasmi, na kutakiwa kuelekea kwenye maeneo ambayo yametengwa hadi kufikia siku ya ijumaa.
Kufuatia sintofahamu hiyo mapema leo disemba 3 Jijini humo Jeshi la polisi lililazimika kuingilia kati na kutuliza ghasia za wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Mwanjelwa waliokuwa wakipinga agizo la kuwataka waondoke.
Ghasia hizo za wafanyabiashara zimepelekea kufungwa kwa soko hilo baada ya kufunga barabara ya kuelekea hospitali ya Mwanjelwa.