
Sehemu ya athari za ajali hiyo
#HABARI Watu wanaokadiriwa kufika au zaidi ya 50 wanasadikiwa kufa baada ya kuungua na moto kufuatia Lori la mafuta kulipuka eneo la Msamvu mjini Morogoro. Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakiiba mafuta kwenye Lori hilo ambalo lilipata ajali majira ya saa 1:00 Asubuhi leo Aug 10
— East Africa TV (@eastafricatv) August 10, 2019
Lori hilo lilipata ajali majira ya saa 1:00 Asubuhi, ambapo Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Stephen, amefika eneo la tukio na kuthibitisha kuwa miili ambayo imeshahesabiwa ni 54 huku mingine ikiendelea kutolewa katika eneo la ajali.
TAHADHARI PICHA HII INAWEZA IKASUMBUA WATU WENGINE:
Hapa ni eneo la Msamvu Morogoro, ambapo imetokea ajali ya Lori kisha likalipuka kwa moto na kusababisha vifo vya watu wengi. Kinachoendelea sasa ni miili kuondolewa eneo hilo kwaajili ya kuhifadhiwa. pic.twitter.com/sM0LE4UazN
— East Africa TV (@eastafricatv) August 10, 2019
Mh Kebwe ameongeza kuwa baadhi ya majeruhi wamekimbizwa katika hospitali tofauti tofauti kwaajili ya huduma ikiwemo za macho kutokana na mafuta kuwaharibu macho na wengine kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili.
UPDATES
#UPDATES Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Wilbrod Mtafungwa, amesema mpaka sasa miili 61 imetolewa na zoezi bado linaendelea, hivyo atatoa taarifa zaidi baadaye. pic.twitter.com/DjMHWWatyq
— East Africa TV (@eastafricatv) August 10, 2019
#UPDATES Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Morogoro, Rita Lyamuya amesema mpaka sasa wameshapokea majeruhi 60, ambao kati yao wanaume ni 58 huku wanawake wakiwa ni wawili. #AjaliMorogoro
— East Africa TV (@eastafricatv) August 10, 2019
UPDATES: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa pole kwa familia za marehemu.
Pole kwa wafiwa wote.
Marehemu mpumzike mahali pema peponi.
Majeruhi mpone haraka. pic.twitter.com/pPMmqOB9Ha— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) August 10, 2019