Ijumaa , 18th Aug , 2023

Watu 10 wamefariki dunia hii leo Agosti 18, 2023, katika ajali iliyohusisha gari dogo la mizigo (kirikuu) na gari la Polisi maeneo ya Dutch Corner Siha mkoani Kilimanjaro umbali wa kilomita 50 kutoka mjini Moshi.

Magari yaliyopata ajali

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka tairi la kirikuu kisha kuhama barabara na ndipo magari hayo yalipokutana uso kwa uso. 

Hospitali ya Kibong'oto imethibitisha kupokea miili ya watu 10 na miongoni mwao saba ni wanawake.