
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea mara baada ya mwanaume huyo kutoka hospitali kwa kwaajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua na kueleza kuwa amekata tamaa ya kupona na kuamua kujikata uume wake.
Aidha kamanda Mutafungwa amesema kwa sasa mgonjwa huyo anapatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo kutokana na kitendo alichofanya cha kujijeruhi na pindi atakapopona jeraha lake atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.