Jumapili , 23rd Jun , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli amehani msiba kwa Bw. Abbas Tarimba Abbas ambaye hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam.

Alipofika nyumbani hapo Rais Magufuli aliendesha ibada ya kuwatia moyo familia ya Abbas Tarimba ambaye amepoteza watoto wake wawili.

Mapema leo asubuhi Mhe rais Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es salaam, katika Misa Takatifu ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu kanisani hapo.

Kujionea zaidi tazama video hapo chini.