Amuua mke mwenza na kumzika shambani

Alhamisi , 14th Dec , 2017

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP), Augustine Ollomi amesema picha zinazoendelea kusambaa mtandaoni zikionyesha askari Polisi wilayani Ngara Mkoani Kagera wakishirikiana na wananchi kufukua mwili

Maaskari wakifukua mwili wa Noelina aliyeuliwa na mke mwenza

wa marehemu Noelina Joseph mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa  kijiji cha mayenzi wilayani humo ni tukio la kweli.

Noelina Joseph (24) mkazi wa kijiji cha Mayenzi wilayani humo ameuawa na mke mwenza jana aliyejulikana kwa jina la Edina na kuzikwa kwenye shamba la viazi kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya kuolewa na mume mmoja kijini humo

“Ni kweli tukio hilo limetokea huko Ngara na tayari maafisa wetu wapo eneo la tukio ila bado uchunguzi zaidi haujafanyika ndio tunaendelea nao” ,amesema kamanda Ollomi.

Wawili hao ni wake wa Joseph Laurean (33), mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara.

Mke mkubwa, Edina alihisiwa kuhusika na mauaji baada ya mumewe kumkuta akiwa na damu mwilini shambani.

Mume wa wake hao Bwana Laurian, alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ndipo mtuhumiwa Edina alipohojiwa na alieleza alikuwa na chuki na mke mwenzake aliyeolewa miezi miwili iliyopita.

Edina akiwa chini ya ulinzi na aliwapeleka kwenye shamba la mume wake ambalo ni mali ya binamu yake John Shimimana alikoonyesha alikomzika mwenzake kwenye tuta la viazi.

Tukio hilo la kufukua mwili wa marehemu limefanyika kuanzia mida ya asubuhi ya leo baada ya kugundulika na watu na taarifa hizo kutolewa Polisi na baadaye kujulikana aliyefanya kitendo hicho ni mke mwenza wa marehemu Noelina

 Mke mwenza anayetuhumiwa kufanya tukio hilo akiwa chini ya ulinzi wa polisi