Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amethibisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mtu huyo amekutwa umeuawa huku mwili ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kifuani.
Kutokana na tukio hilo Kamanda Mkama amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi huku mtuhumiwa akitafutwa na mara baada ya kupatikana na upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.
Mbali na tukio hilo pia Kamanda Makama amesema katika maeneo ya Msamvu Manispaa ya Morogoro jeshi hilo limeokota miili miwili ya watoto (mapacha) ambao imetokana na kutolewa kwa mimba ambayo haijafikia umri na kisha kutupwa eneo la karibu na kituo cha mabasi msamvu.




