Jumanne , 15th Mar , 2016

Zaidi ya waendesha pikipiki mia moja na thelathini katika kata ya Tingatika wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha wamepatiwa mafunzo ya Polisi jamii na udereva ikiwa ni katika jitihada za kupunguza uhalifu.

Waendesha bodabodo wa Jijini Arusha

Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Shirika la kupunguza umaskini Tanzania (APEC)ambao ndio waendeshaji wa mafunzo hayo Respucius Timanywa,amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia madereva wa bodaboda ambao ndio wanotajwa zaidi kuhusika katika vitendo vya uhalifu na kutakiwa kushiriki katika ulinzi wa jamii.

Nae mkuu wa polisi wilaya ya Longido, John Hadu amesema mafunzo hayo licha tu ya kupunguza ajali yatasaidia kuongeza ulinzi kwa jamii kwani jeshi la polisi pekee haliwezi kuimarisha ulinzi pasipo ushiriki wa wananchi.

Nao baadhi ya washiri wakiwemo madereva wamesema kwa sasa baada ya kupatiwa mafunzo hayo watakuwa mstari wa mbele kwa kufuata sheria za barabarani.

Mpaka sasa shirika la Apec limewapatia zaidi ya wananchi laki moja mafunzo ya udereva na ulinzi shrikishi ikiwa ni sehemu ya sera yake ya kupunguza umaskini.