
Jengo la Bodi ya Mikopo
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, Mkuu wa Mawasiliano ya Bodi hiyo, Omega Ngole amesema kuwa wanaufaika wengi wamekuwa wakijificha pindi wanapohitimu elimu hiyo ya juu, hivyo kuisababishia hasara bodi na kupelekea wanafunzi wengi kukosa mikopo.
Aidha Omega ameongeza kuwa makato hayo ya asilimia 15 yanayopingwa na baadhi ya wadau nchini, yamefanya bodi ikusanye marejesho ya Shilingi Bilioni 18.9 ndani ya mwezi mmoja.