.gif?itok=-CkWlFzj×tamp=1472835183)
Msimamizi na mshauri wa programu ya Uwezo Prof. Kitila Mkumbo.
Mbali na hilo, utafiti umeonesha kuwa watoto wawili kati ya kumi hawajui kusoma kiswahili na hesabu jambo ambalo serikali inapaswa kuongeza juhudi katika kuboresha elimu nchini.
Takwimu hizo zimetolewa na Msimamizi na Mshauri wa Programu ya Uwezo Prof. Kitila Mkumbo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa utafiti huo umefanyika kwa watoto walio majumbani na mashuleni kwa wilaya zote nchini Tanzania.
Prof. Mkumbo amesema kwa mujibu wa utafiti huo inaonesha kuwa sababu kubwa ya matokeo hayo ni pamoja na wazazi kutokuwa wafuatiliaji wa maendeleo ya watoto wao pamoja na mahudhirio mabovu ya walimu kuingia madarasani.
Aidha Prof. Kitila ameongeza kuwa tafiti nyingine zinaonesha kuwa hata uwezo na maarifa ya baadhi ya walimu katika stadi zao katika kufundisha wanaonekana hawana uwezo wa kufundisha masomo hayo.
Amesema kuwa walimu wengi wanaofundisha masomo ya Hesabu, Kiingereza pamoja na maarifa ya jamii baadhi yao uelewa wao uko chini kwa mujibu wa utafiti uliotolewa hivi karibuni na benki kuu ya dunia ulibainisha hivyo