Jumanne , 2nd Jul , 2019

Kesi namba 112 ya mwaka 2018 inayowakabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho imeahirishwa leo Juni 2 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Viongozi mbalimbali wa CHADEMA

Kesi hiyo inayowajumuisha Ester Matiko, John Mnyika na Grace Kiwelu inayohusu kufanya mkusanyiko usio halali, imeahirishwa baada ya shahidi wa 6, Koplo Charles kuzidiwa akiwa kizimbani.

Akiongozwa na wakili wa serikali Kadushi kutoa ushahidi wake, Dengue yatajwa kuwa sababu ya kesi hiyo Kuahirishwa.

Shahidi Koplo Charles alizidiwa akiwa Kizimbai ambapo alidai hajisikii vizuri baada ya kulazwa wiki iliyopita akisumbuliwa na Ugonjwa wa Dengue

Baadhi ya mashtaka waliyosomewa ni kula njama na kufanya mkusanyiko usio halali, wenye ghasia na kukiuka tamko la kutawanyika na kusababisha watu waogope. Tukio hilo lilifanyika Februari 16, 2018 katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni Jijini Dar es salaam.