
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Philip Mpango.
Jina hilo limewasilishwa bungeni kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mpambe wa Rais na kusomwa na Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai.
Tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha jina la aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi huo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati. Dk. John Pombe Magufuli na aliyekuwa Makamu wake Mhe. Samia Suluhu Hassan kuapishwa kushika nafasi ya Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kufanya nafasi ya Makamu wa Rais iwe wazi na leo kujazwa rasmi.