Jumanne , 11th Oct , 2022

Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kundi la kijiografia Kanda ya Afrika ya Umoja wa Mabunge Duniani (African Geopolitical group of IPU) .

Dk Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza uteuzi huo umefanyika jana Jumatatu Oktoba 10,2022 na wajumbe wa kundi hilo katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Kigali (KCC) nchini Rwanda katika Mkutano wa 145.

Dk Tulia ambaye ataongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja pia ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya uongozi wa makundi ya kijiografia (IPU) nafasi ambayo imeelezwa kuwa ni ya juu kati ya nafasi za Umoja wa Mabunge Duniani kwa mujibu wa kanuni za uongozi wa umoja huo.