Alhamisi , 17th Jan , 2019

Kwa siku ya pili mfululizo tangu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla alivyofanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu, kumekuwa na gumzo juu ya kiatu alichovaa katika mazungumzo hayo.

Rais Magufuli akitoka Ikulu pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega

Januari 15, Waziri Kigwangalla alialikwa na Rais Magufuli kufanya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es salaam, lakini mshangao wa wengi ni katika picha alipokuwa akitoka nje na Rais Magufuli, iliyoonesha kiatu chake kikiwa na vumbi kali lililoziba rangi ya kiatu hicho.

Mwenyewe amesimulia namna mazingira yalivyokuwa hadi kupelekea kiatu chake kufunikwa na vumbi ilhali alikuwa ameitwa na Rais Ikulu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kigwangalla ameandika kuwa.

 

Pia wakati akitoka kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu, sambamba na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga, aliandika.