Jumanne , 31st Mei , 2022

Hukumu ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sebaya, imeahirishwa hadi Juni 10, 2022, kwa kile kilichoelezwa kwamba Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo amepangiwa majukumu mengine ya kiofisi nje ya mkoa.

Lengai Ole Sabaya

Kesi hiyo imeahirishwa leo Mei 31, 2022, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha Fadhili Mbelwa.

Hukumu ya leo dhidi ya Sabaya na wenzake sita, ilitarajiwa kuamua hatima ya kiongozi huyo wa zamani na wenzake endapo wataachiwa huru, kwa kuwa baada ya kesi hii hawana nyingine iliyosalia mahakamani.