Jumanne , 22nd Dec , 2020

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, amefanya ziara ya kustukiza usiku wa manane kwenye ujenzi wa soko la Tandale kwa lengo la kujionea kama maagizo aliyotoa yametekelezwa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge.

Miongoni mwa maagizo aliyotoa RC Kunenge kwenye ziara aliyofanya Desemba 19, 2020, ni pamoja na kumtaka mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana na kuongeza idadi ya vibarua na kukuta mkandarasi huyo ametekeleza agizo kwa kufunga taa na anafanya kazi ya kumwaga zege, ambapo amemuelekeza kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kabla ya mwezi wa nne mwakani.

Aidha RC Kunenge ametuma salamu kwa wakandarasi wote wanaotekeleza miradi jijini humo kuzingatia mikataba yao kwa kuhakikisha, wanakamilisha miradi kwa wakati ili iweze kutatua kero za wananchi kama serikali ilivyokusudia.